Corciolli - Ulimwengu (feat. Vini Ngugi & Eric Wainaina)
Translated lyrics of Corciolli - Ulimwengu (feat. Vini Ngugi & Eric Wainaina) to
- 106 hits
- Published 2024-08-28 00:00:00
- 0 Comments
- 0 likes
- Corciolli
- Ulimwengu (feat. Vini Ngugi & Eric Wainaina)
- Translation by: panzas
Ulimwengu (feat. Vini Ngugi & Eric Wainaina)
Tunapojituma
Kuyaharibu makaazi yetu
Tunajihatarisha
Bila shaka twajiangamiza
Muda wetu wayoyoma
Kadri unavyosonga
Tunajiteketeza
Misitu ikiisha utavutaje mvua
Jukumu letu kuelewa
Kuwa jua, mwezi, mvua na ardhi
Wanyama pori na adinasi
Mito, milima, misitu na nyasi
Vidudu na ndege wa angani
Vimefumwa kwa pamoja
Ulimwengu ukizunguka
Kile tunachopanda
Bila shaka ndicho tutavuna
Kama jua likitua
Yale tunayofanya
Bila shaka yatatufuata
Binadamu ni tishio kubwa kwa dunia
Na vitendo anavyo fanya
Hufanya viumbe kuumia
Sasa chukua hatua
Wakati ndio sasa
Kuyahifadhi mazingira
Kupata amani
Twahitaji uwiano
Kuilinda dunia
Kwa vizazi vijavyo
Ulimwengu ukizunguka
Kile tunachopanda
Bila shaka ndicho tutavuna
Kama jua likitua
Yale tunayofanya
Bila shaka yatatufuata
Por el momento, a nadie le gusta este artículo
Comments
Hey! You're in luck, no one has commented on this article yet. Be the first one and leave your comment.
You need to be registered to leave comments.
Log in with your user account and enjoy all the benefits.
Create your account ó Sign in / Log in